Wednesday, February 15, 2012

UNAFIKI HUU WA WANASIASA WETU HADI LINI

Mwaka 2008, baada ya kuibuka kwa kashfa ya kampuni hewa ya richmond, watanzania tuliamini kuwa ukombozi wa kweli umepatikana kwani wabunge wengi walionesha uzalendo wa hali ya juu kwa kujadili kuhusu kashfa ya richmond na kuunda kamati teule kuchunguza kampuni ya richmond. Kamati teule baada ya uchunguzi, ilibaini kuwa kampuni ile ilikuwa hewa au ya mfukoni. Wabunge wengi wakatoa machozi yao kuonesha uchungu walionao kwa rasilimali ya wananchi wa tanzania.
Mfano wabunge kama vile: Anne kilango, Samwel Sitta, Harrison mwakyembe, na wengine wengi walichukizwa sana na ufisadi uliofanywa kupitia kampuni ya richmond.
Imani ya watanzania kuwa wabunge wao ni wazalendo, ilianza kufifia baada ya kugundua kuwa kashafa mbalimbali za ufisadi zilizokuwa zikiibuliwa ikiwamo hii ya richmond hazikushughulikuwa. Imani hiyo ilitoweka kabisa mwaka jana baada ya wabunge walewale wa ccm ambao mwaka 2008 walionesha uzalendo kwa kuchukia ufisadi, kupitisha muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 bila kujali matakwa ya watanzania. Tuliona kuwa wabunge wa chadema na nccr mageuzi walipotoka nnje ya ukumbi wa bunge ili kupinga muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba,wale wa ccm wakaanza kuupitisha kwa mbwembwe nyingi huku wakionesha madharau kwa wabunge wa upinzani. Hapo ndipo tulipobaini kuwa wabunge wetu ni wanafiki wakubwa kwani wanapuuza matakwa ya wapiga kura wao. Ajabu mwaka huu mwezi wa pili mheshimiwa rais pamoja na kusaini ule muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba mwaka jana akawasilisha mabadiliko ambayo wabunge wa chadema waliyataka. Wabunge wa ccm walichukia sana kitendo kile kwani mwaka jana wapinzani walipotoka nnje ya ukumbi wa bunge kupinga muswada huo, wao waliwacheka kwa hiyo ilikuwa aibu kubwa kwao. Haikutegemewa kabisa kuwa wabunge kama akina Kilango na wenzake waliokuwa wakitoa machozi bungeni kutokana na ufisadi uliofanywa kupitia kampuni ya richmond leo wangekuwa mstari wa mbele kutetea mambo ambayo hayana maslahi kwa umma. Hii inaonesha ni jinsi gani wanasiasa wana ndimi mbili. Yaani unafika uliokithiri. Unafiki huu hadi lini?

No comments:

Post a Comment